Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Burundi leo wanapiga kura katika uchaguzi wa madiwani

Wananchi wa Burundi leo wanapiga kura katika uchaguzi wa madiwani

Wananchi wa Burundi leo wamepiga kura katika uchaguzi wa madiwani, ikiwa ni mwanzo wa mchakato wa uchaguzi mkuu wan chi hiyo utakaofuatiwa na uchaguzi wa rais na wabunge.

Wananchi milioni 3 na laki sita wanashiriki uchaguzi wa leo na tume ya uchaguzi imesema hakuna matatizo makubwa katka upigaji kura. Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo amewasihi wagombea wote kukubali matokeo yatakavyokuwa.

Uchaguzi huu una umuhimu mkubwa wa kuonyesha umaarufu na nguvu za vyama wakisubiri uchaguzi wa Rais hapo Julai. Mkoani Ngozi Kaskazini mwa nchi hiyo ndiko anakotoka Rais wa sasa Pierre Nkurunziza na ndiko alikopiga kura yake na kupuuza madai ya watu kuwa kuna hofu ya kuzuka vita katika uchaguzi huu.