Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa haki za binadamu aelekea Burundi katika maandalizi ya uchaguzi

Mtaalamu wa haki za binadamu aelekea Burundi katika maandalizi ya uchaguzi

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu kwa ajili ya Burundi Akich Okola atafanya ziara nchini Burundi kuanzia kesho kutwa Mai 23 hadi 29 kutathmini haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu wan chi hiyo.

Okola amesema uchaguzi huu utakaoanza na wa madiwani Jumatatu ya tarehe 24 Mai ni wa pili wa kidemokrasia tangu kutiwa saini mkataba wa amani wa Arusha mwaka  2000. Ameongeza kuwa Burundi sasa hivi iko katika wakati muhimu hivyo mashauriano kati ya serikali na wadau wengine ni muhimu ili kuhakikisha unafanyika uchaguzi wa amani, kidemokrasia na utakaozingatia haki za binadamu.

Okola amesema wakati wa ziara hiyo atapokea taarifa kuhusu haki za binadamu inayoambatana na uchaguzi ,kama vile uhuru wa kufanya mikutno, uhuru wa kujiunga na kundi lolote na uhuru wa kujieleza.