Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya Ban kuhusu watoto kwenye migogoro imewataja wadhalimu

Ripoti ya Ban kuhusu watoto kwenye migogoro imewataja wadhalimu

Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu watoto kwenye nchi za migogoro ya kutumia silaha imejumuisha wadhalimu wanaowadhalilisha na kuwatumia watoto.

Ripoti hiyo iliyofanyiwa kazi kwa miaka mitano imewataja wanaowapa mafunzo ya vita na kuwatumia watoto jeshini katika mapigano. Pia miongoni mwa vitu muhimu vilivyomo kwenye ripoti hiyo ni fursa iliyotolewa na kupitishwa kwa azimio la baraza la usalama namba 1882 mwaka 2009.

Azimio hilo limeruhusu kuzitaja na kuziaibisha nchi na zisizo nchi na makundi ambayo yameuwa, kubaka na kutumia ukatili wa kimapenzi dhidi ya watoto. Baadhi ya nchi zilizotajwa ni kama Ufilipino, Thailand, Myanmar, Chad , Sudan na Colombia huku makundi ya waasi kama LRA kutroka Uganda na FDLR walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanalaumiwa.