Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu kwa wapenzi wa jinsia moja Malawi ni ubaguzi:Pillay

Hukumu kwa wapenzi wa jinsia moja Malawi ni ubaguzi:Pillay

Uamuzi wa serikali ya Malawi kuwahukumu kwenda jela miaka 14 na kazi ngumu wanaume wawili wanaodaiwa kufanya vitendo kinyume na utamaduni umelaaniwa na Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amesema kwamba hukumu hiyo ya miaka 14 kwa wapenzi hao wa jinsia moja nchini Malawi ni ya kibaguzi na inatoa ishara mbaya katika eneo hilo hasa kwa jinzi wanavyowatendewa mashoga, wasagaji, wanaoshiriki mapenzi ya pande zote na makundi yanayowaunga mkono.

Ametoa wito wa kubadilishwa kwa hukumu hiyo na sheria zinachukulia mapenzi ya jinsia moja kama kosa la jinai zifanyiwe marekebisho. Amesema kwa kifupi ameshitushwa sana na hukumu hiyo.