Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washiriki ufadhili wa mkutano wa kimataifa wa kuisaidia Somalia

UM washiriki ufadhili wa mkutano wa kimataifa wa kuisaidia Somalia

Mkutano wa siku tatu utakaojadili masuala muhimu ya hatma ya Somalia umeanza leo mjini Istanbul Uturuki.

Masuala hayo muhimu ni pamoja na ushirikiano wa kisiasa, usalama, ujenzi mpya wan chi hiyo iliyoharibiwa na miongo miwili ya vita na suala la maendeleo. Mkutano huu unajikita katika mada hizo kama sehemu ya ya utekelezaji wa maafikiano ya amani ya mwaka 2008 yajulikanayo kama Djibout Peace Accord.

Viongozi wa ngazi za juu kutoka nchi 55 wanahudhuria mkutano huo akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye akihutubia kwenye chuo kikuu cha Bogazici mjini Istanbul kwenye ufunguzi wa mkutano huo amesema dunia inabadilika na Uturuki inakwenda nayo sambamba.

Pia ameongelea umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa kupambana na magonjwa, mabadiliko ya hali ya hewa na silaha za maangamizi. Wengine watakaohutubia mkutano huo ni waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip edogan na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh ahmed.