Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa afya unalenga kutokomeza surua 2015

Mkutano wa kimataifa wa afya unalenga kutokomeza surua 2015

Shirika la afya duniani WHO linasema juhudi za kutokemeza surua zimepigwa kumbo na ugonjwa huo umeanza kurejea kwa kasi.

Shirika hilo linasema kupungua kwa fedha na kutokuwepo na wajibu wa kisiasa kumesababisha kuzorota kwa juhudi za kutokomeza surua. WHO inasema vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano kutokana na surua vimepungua kwa asilimia 89kutoka milioni 1.1 mwaka 1990 hadi kufikia 118,000 mwaka 2008.

Hata hivyo kuzuka upya kwa ugonjwa huo katika nchi 31 za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara, Uingereza, Bulgaria, Indonesia, Philipines, Thailand na Vietnam mwaka mmoja uliopita kumetia dosari juhudi za kuumaliza ugonjwa huo.

Lajkini katika mkutano wameafikiana kufikia malengo ya asilimia 90 ya chanjo ifikapo 2015. Dr Peter Strebel ni kutoka kitengo cha chanjo cha WHO