Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kuwepo Afghanistan lkutoa msaada

Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kuwepo Afghanistan lkutoa msaada

Umoja wa Mataifa una lengo la kusalia Kusini mwa Afghanistan licha ya hali duni ya usalama katika eno hilo . Azimio hili limetolewa na mjumbe wa Umoja wa Mataiafa nchini humo Steffan de Mistura.

De Mistura amesema Umoja wa Mataifa umekuwa nchini Afghanistan kwa muda na hususani katika enoe la Kusini mwa nchi hiyo na utazidi kuwepo ili kuwasaidia watu wa Kandahar wakati mambo yanapokuwa magumu.

De Mistura ambaye pia ni mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Afghanistan, UNAMA amekuwa katika ziara ya siku moja katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo ili kujionea hali ilivyo na kukutana na baadhi ya viongozi wa mashinani na wafanyi kazi wa Umoja wa Mataifa.