Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO imelaani mauaji ya waandishi wa habari Somalia na Pakistan

UNESCO imelaani mauaji ya waandishi wa habari Somalia na Pakistan

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ,UNESCO amelaani mauaji ya hivi karibuni ya waandishi wa habari nchini Somalia na Pakistan, akisisitiza kuwe[po uhuru wa waandishi wa habari.

Mtangazaji wa muda mrefu wa radio, Shekh Nur Abkey alitekwa nyara mnamo May 4 akiwa njiani kwenda nyumbani akitokea kazini katika radio inayomilikiwa na serikali na kisha kupigwa risasi na kuuwawa. Mbali na hayo yeye amekuwa akiwafunza waandishi chipukizi katika radio hiyo ambayo inaonekana kuyashutumu vikali makundi ya kiislamu nchini humo.

Mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova amesema kifo chake ni kitendo cha kinyama na ni uhalifu dhidi ya mwandishi wa habari na jamii ya Wasomali kwa ujumla.