Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa Darfur hauwezi kumalizwa kwa mtutu wa bunduki:Gambari

Mgogoro wa Darfur hauwezi kumalizwa kwa mtutu wa bunduki:Gambari

Mgogoro katika eno la Darfur hauwezi kutatuliwa kwa kutumia nguvu za kijeshi bali kwa amani na njia ya mashauriano.

Tathmini hii imetolewa leo na mjumbe maalum wa juhudi za pamoja za kutafuta amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID, Ibrahim Gambari katika taarifa yake kwa waandishi wa Habri hapa New York.

Gambari ameelezea wasi wasi wake kuhusu mapigano makali kati ya wanajesi wa serikali na waasi pia mapigano kati ya jamii mbali mbali za Darfur ambapo, amesma yameathiri pakubwa raia, huku wengine wakiachwa bila makazi na hivyo kuwa vigumu kupelekwa kwa misaada kwa wale walioathirika.