Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuhusu kuzama kwa meli ya Korea Kusini ni ya masikitiko:Ban

Ripoti kuhusu kuzama kwa meli ya Korea Kusini ni ya masikitiko:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa kauli baada ya kupokea ripoti ya kuhusu kuzama kwa meli ya wanamaji wa Korea Kusini Machi 26 na kuua mabaharia 46 wa nchi hiyo.

Ban Ki-moon amesema ripoti hiyo "inatatiza." Kwa mujibu wa msemaji wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu amepokea matokeo ya uchunguzi wa kuhusu kuzama kwa meli hiyo ya Cheonan ya Jamuhuri ya Korea kwa moyo mzito na akiwa na hofu kubwa.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo baada ya ripoti hiyo. Pia inasema Ban ameshukuru staha na juhudi za uvumilivu za serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuchunguza tukio hilo kwa makini na ustarabu wakitumia wataalamu wa ndani na wakimataifa.