Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa ombi la kimataifa kuwasaidia waathirika wa mafuriko Tajikistan

UM umetoa ombi la kimataifa kuwasaidia waathirika wa mafuriko Tajikistan

Umoja wa Mataifa hii leo umetoa ombi kwa jamii ya kimataifa la dola milioni 5.3 kuisaidia serikali ya Tajikistan ili kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika na mafuriko kusini mwa taifa hilo la Asia ya kati.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa , OCHA nchini humo watu walioathirika na mafuriko katika taifa hilo masikini zaidi kati ya mataifa yaliyokuwa muungano wa Urusi wanatarajia usaidizi wa kimataifa ilikurejea heshima yao na kuepuka wasiwe masikini zaidi.

Watu 40 wamekufa, huku wengine 33 hawajulikani waliko. Na watu 85 wamejeruhiwa vibaya kutokana na mafuriko hayo. Wakati huo huo takriban watu 4,500 wameachwa bila makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko katika eneo la Kulya tarehe 7 May.