Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP leo imezindua mpango wa kazi kwa chakula kuwasaidia Wairaq

WFP leo imezindua mpango wa kazi kwa chakula kuwasaidia Wairaq

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP, limezindua mpago wa kazi kwa chakula ili kuwasaidia raia masikini wa Iraq kupata fedha za kutosha za kununua chakula.

Programu hiyo pia inaanzishwa katika wilaya ya Kati ya Iraq ya Diyala ili kuwapa watu ajira na kuhakikisha kuwepo kwa usalam katika maeneo Wilaya yaliyo na umasikini mwingi.

Baadhi ya shughuli ya pesa kwa chakula ni kusafisha mabwawa ya kupitisha maji machafu, upandaji wa miti na usafi. Na washirki wa shughuli hiozo wanalipwa dola 10 kwa siku kwa muda wa miezi mitatu huku wasimamizi wakilipwa dola 13.