Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la UM lajadili amani na usalama barani Afrika

Baraza la usalama la UM lajadili amani na usalama barani Afrika

Njia mbili pekee za kuleta amani nausalama nchini somalia ni kuudhibiti mji wa Moghadishu na viunga vyake kutoka kwa wanamgambo wenye itikadi kali.

Pendekezo hilo limetolewa na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh katika taarifa yake kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa ambalo leo limekuwa likijadili amani na usalma barani afrika. Kiongozi huyo wa Djibouti ameonya kwamba serikali ya mpito ya Somalia inadhoofika haraka kutokana na kuanza kuzidiwa nguvu na wanamgambo karibu nchi nzima.

Amelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuamua kuchukua udhibiti wa Mogadishu, kurejesha utawala wa sheria, utulivu na huduma wakati mashirika ya Umoja wa Mataifa na mengine yasiyo ya kiserikali yakianza kurejea Moghadishu. Amesema ukweli ni kwamba bila kudhibiti Moghadishu basi serikali ya mpito haiwezi kuwa na udhibiti wa nchi hiyo. Amesisitiza kwamba hatua hii inahitaji mabadiliko ya mtazamo wa baraza la usalama na sekretariati ili kuchukua hatua ya kuikomboa Somalia moja kwa moja.