Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mswada dhidi ya nyuklia ya Iran wawasilishwa kwenye baraza la usalama

Mswada dhidi ya nyuklia ya Iran wawasilishwa kwenye baraza la usalama

Marekani imewasilisha mswada wa azimio kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutaka vikwazo zaidi dhidi ya Iran kutokana na mipango yake ya nyuklia.

Mswada huo ambao waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ameuita ni mzito na wenye nguvu umewasilishwa siku chache tuu baada ya Iran kuwa na maafikiano na Brazilin a Uturuki ambapo Iran imekubali kupeleka madini ya uranium Uturuki kwa malipo ya mafuta kwa ajili ya utafiti.

Brazil na Uturuki wote wako kwenye kikao cha baraza la usalama na kuna taarifa kwamba Urusi ambayo awali haikutaka kuwa upande wa Marekani sasa pamoja na Uchina wanaunga mkono pendekezo la azimio la Marekani.