Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TB lazima ishughulikiwe kama tatizo la kimaendeleo:The Lancet

TB lazima ishughulikiwe kama tatizo la kimaendeleo:The Lancet

Imebainika kwamba watu zaidi ya tisa kati ya kumi wenye kifua kikuu ugonjwa unaouwa watu milioni 1.8 kila mwaka wanaweza kuepuka kifo kwa kuwepo na vipimo bora, dawa na chanjo.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa tathimini iliyotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza The Lancet, ambapo pia limesema matibabu tangu mwaka 1995 hadi 2008 yameokoa maisha ya watu milioni sita waliokuwa na kifua kikuu.

Lakini jarida hilo linasema kifua kikuu unasalia kuwa ni ugonjwa unaoua watu wengi zaidi na kushindwa kupata fedha zinazohitajika kukabiliana nao kama magonjwa mengine yanayokatili maisha ya watu wengi. Asilimia 80 ya kifua kikuu hukuma mataifa 22 na 11 yakiwa barani Asia na tisa yakiwa Afrika na Urusi. Mkurugenzi mkuu wa Lancet Pam Das amesema kwa muda mrefu mtazamo wa kukabiliana na kifua kikuu umekuwa ni kutibu ugonjwa huo kama tatizo la kawaida la kiafya hatua ambyo haitoshi