Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la uharamia haliwezi kutatuliwa baharini tuu asema Ban Ki-moon

Tatizo la uharamia haliwezi kutatuliwa baharini tuu asema Ban Ki-moon

Uharamia unaweza kuwa ndio uhalifu wa kwanza wa kimataifa na juhudi za kupambana nao zimefanya kuwe na sheria za kwanza za kimataifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa usio rasmi kuhusu uharamia baharini na ukijikita katika hali ya Somalia na tatizo hilo. Katibu Mkuu amesema wakati Umoja wa Matifa una haki ya kisheria kuwa msingo wa mapambano dhidi ya uharamia duniani mashambulizi dhidi ya vyombo vya usafiri, meli za mafuta na meli za uvuvi yanaendelea na yameongezeka katika miaka ya karibuni akisisitiza kuwa uharamia , unamea mizizi.

Bwana Ban ametaja mambo manne ya kukabiliana na uharamia miongoni mwao ni ushirikiano wa kimataifa ambao amesema ni muhimu sana kwani uharamia hauwezi kutatuliwa baharini tuu na washukiwa wa uharamia lazima wafikishwe kwenye mkono wa sheria. Pia amesema jambo lingine ni kuuangalia uharamia kwa mapana hasa suala la usalama baharini .

Amesema kuna mambo mengi yanayoingiliana na uharamia kama usalama wa makontena, usafirishaji haramu wa watu, uhalifu wa kupangwa na usambazaji wa fedha haramu.Hivyo uharamia hauwezi kumalizwa bila kushughulikia uhalifu huu kwanza.