Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu wa UM yuko Cameroon kwa mkutano kuhusu Afrika

Naibu Katibu Mkuu wa UM yuko Cameroon kwa mkutano kuhusu Afrika

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro leo na kesho yuko ziarani mjini Yaunde Cameroon kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu Afrika.

Mkutano huo unaangazia changamoto za maendeleo katika bara la Afrika na umeandaliwa na serikali ya Cameroon ambayo pia inaadhimisha miaka 50 tangu kupata uhuru.

Viongozi mbalimbali wa Afrika watahudhuria mkutano huo ambapo Asha Rose Migiro anatazamia kuhutubia juu ya changamoto zinazoikabili Afrika na mchango wa Umoja wa Mataifa katika kulisaidia bara hilo.