ICRC inasaidia imesaidia kuhamisha wafungwa walioachiliwa na JEM Sudan
Kamati ya kimataifa ya chama cha msalanba mwekundu ICRC leo imesaidia kuwaweka huru na kuwasafirisha wanajeshi wa Sudan 44 na kuwakabidhi kwa serikali ya nchi hiyo mjini Alfasher kwenye jimbo la Darfur.
Wanajeshi hao walikuwa wanashikiliwa na kundi la Justice and equality Movement JEM na wameachiliwa kama sehemu ya JEM kutekeleza mpango wa makubaliano na serikali yalityotiwa saini mjini Doha mwezi Februari mwaka huu.
Kwa mujibu wa Jordi Raich Circo mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Sudan, baada ya kuombwa na pande zote ICRC ilikubali katika misingi ya kibinadamu kuwa mpatanishi na kufanikisha operesheni hiyo ,ingawa amesema haikushiri katika majadiliano ya kuachiwa huru kwa watu hao.
ICRC pia imesema imepata msaada mkubwa wa kiufundi kutoka kwa WFP kuhakikisha shughuli hiyo inafanikuiwa bila purukushani yoyote. Pia iliwahoji mateka hao mmojammoja ili kuhakikisha wanakabidhiwa kwa kamati hiyo kwa hiyari yao bila shuruti.