Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama limehitimisha ziara Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Baraza la usalama limehitimisha ziara Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamehitimisha ziara yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ziara hiyo ilikuwa ni ya kutathimini hali halisi na pia kutanabahi hatma ya mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUC ambao muda wake utakamilika hivi karibuni.

Wakiwa nchini Congo kiongozi wa msafara balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud amesema ujumbe huo ulipata fursa ya kukutana na Rais Joseph Kabila, waziri mkuu Adolphe Muzito na viongozi wa bunge nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa Bwana Araud alisema mazungumzo yameanza na serikali, jumuiya za kijamii na umma juu ya hatma ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuwepo nchini humo. Ameongeza kuwa ujumbe wake na serikali ya Congo wameafikiana kuwa majadiliano zaidi ya hatma ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo yanahitajika.