Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana kutoka Gaza washinda tuzo na kukutana na Ban Ki-moon

Wasichana kutoka Gaza washinda tuzo na kukutana na Ban Ki-moon

Wasichana watatu kutoka shule inayoendeshwa na shirika la misaada la Umoja wa Mataifa kwa Wapalestina UNRWA kwenye kambi ya wkimbizi ya Askar mjini Nablus wameshinda tuzo ya mashindano ya dunia ya sayansi kwa vijana.

Wasichana hao wameandika historia kwa kuwa Wapalestina wa kwanza kushinda tuzo ya mashindano hayo. Wasinana hao wenye umri wa miaka 14 kila mmoja wameshinda tuzo hiyo baada ya kuunda fimbo ya umeme iliyo na hisia kwa watu wasioona ambayo inatoa ishara chini na mbele ywakati wa kutembelea.

Aseel Abdu Elei, Noor alarada na Aseel Ashaar walipokea tuzo yao katika maonyesho ya sayansi San Jose Califonia ambako walishindana na vijana wengine 1500 kutoka kote duniani. Leo wamekunana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Noor Alarada ameiambia radio hii nini kiliwashawishi kuunda fimbo hiyo.