Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umelaani shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya NATO Afghanistan

UM umelaani shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya NATO Afghanistan

Afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amelaani vikali shambulio la kijitoa muhanga mjini Kabul lililokatili maisha ya watu zaidi ya kumi.

Kwa mujibu wa duru za habari nchini humo shambulio hilo lilitokea mapema leo wakati wa pilika nyingi, ambapo mtu wa kijitoa muhanga aliwa kwenye gari lililosheheni mabomu alishambulia msururu wa vikosi vya NATO.

Miongoni mwa waliokufa katika shambulio hilo ni raia wa Afghanistan na wanajeshi wa kimataifa, huku watu wengine wengi wakijeruhiwa. Katika taarifa yake ya kulaani tukio hilo mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura amesema vitendo hivyo vya kikatili na bila sababu vya kuua raia wasio na hatia na wanajeshi wanaoshirikiana na serikali kuhakikisha usalama nchini humo ni lazima vikomeshwe .