Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri wa Kenya ataka wahusika wa machafuko 2007 wapelekwe ICC

Waziri wa Kenya ataka wahusika wa machafuko 2007 wapelekwe ICC

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Lois Moreno Ocampo amekuwa nchini Kenya kuendelea na uchunguzi kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo 2007.

Ocampo ambaye ameahidi kutaja majina ya vigogo sita waliohusika kwa namna moja au nyingine katika machafuko hayo yaliyokatili maisha ya watu zaidi ya 1000 na kuwaacha wengine takribani laki tatu bila makao, amekuwa na mazungumzo pia na serikali ya Kenya.

Waziri wa sheria na katiba wa Kenya Mutula Kilonzo amekuwa hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kukutana na Katibu Mkuu Ban ki-moon ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili sula hilo na ushirikiano unaotolewa na serikali ya Kenya kwa Ocampo.

Bwana Kilonzo akizungumza na mwandishi wa idhaa hii Abdullahi Boru amesema anataka walohusika wawe ni watu wa kawaida au viongozi wapelekwe kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC, ungana nao katika mahojiano haya.