Skip to main content

Ripoti ya UNEP imetoa wito kuongeza uwekezaji katika sekta ya uvuvi

Ripoti ya UNEP imetoa wito kuongeza uwekezaji katika sekta ya uvuvi

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEPimetoa wito wa imetoa wito wa kuwekeza katika ekta ya uvuvi ili kuiimarisha tena sekta hiyo.

UNEP inasema kufanya hivyo kutanufaisha sekta hiyo, walaji na uchumi wa kimataifa kwa kuingiza dola trilioni 1.7 katika miaka 40 ijayo.

Mkuu wa mradi huo wa UNEP Pavan Sukhdev amesema hivi sasa bahari zinazalisha asilimia 10 pungufu ya uwezo wake wa awali na ameonya kuwa kuendelea na kutokuwa na mipango mizuri ya uvuvi kutasababisha kutokuwepo na samaki kabisa katika miaka 40 ijayo.