Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umemtangaza Chriatiana Figuere kuwa mkuu mpya na mabadiliko ya hali ya hewa

UM umemtangaza Chriatiana Figuere kuwa mkuu mpya na mabadiliko ya hali ya hewa

Christiana Figuere kutoka nchini Coasta Rica ametajwa kuwa katibu mkuu mtendaji mpya wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa(UNFCCC).

Christiana anachukua nafasi ya Yvo de Boer anayeondoka.Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa uteuzi huo umefanyika baada ya kushauriana na pande zote za mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa na kitengo husika.

Mapema mwaka huu alipotangaza kugombea nafasi hiyo Bi Figuere akizungumza na waandishi wa habari alisema makataba wa mkutano wa Copenhagen ulikuwa ni hatua kubwa kwa jamii lakini hatua ndoho sana kwa sayari dunia.