Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa um kuhusu elimu ya mtoto wa kike umeanza Senegal

Mkutano wa um kuhusu elimu ya mtoto wa kike umeanza Senegal

Mkutano wa kimataifa unaojadili elimu kwa mtoto wa kike umeanza leo mjini Darka Senegal. Mkutano huo una lengo la kutafuta mbunu mpya za kuhakikisha watoto milioni 56 wengi wao wakiwa wsichana hawakosi haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Mkutano huo ambao pia unaangalia masuala ya jinsia na kuwapa uwezo watoto wa kike katika elimu umeandaliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa elimu kwa mtoto wa kike (UNGEI) ambao unaadhimisha mwaka wa kumi tangu kuanzishwa.

Katika muongo uliopita kumekuwa na mafanikio katika elimu kwa mtoto wa kike, na wasichana wengi na wavulana kwa ujumla wameandikishwa shule duniani kote.

Lakini watoto milioni 56 ambapo zaidi ya nusu yao ni wasichana wanaweza kukosa elimu ifikapo 2015 endapo hali ya sasa itaendelea. Zaidi ya theluithi mbili ya watoto ambao hawasomi hivi sasa wanaishi Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini na magharibi.