Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametoa wito kuchagiza maendeleo ya mawasiliano ya habari

Ban ametoa wito kuchagiza maendeleo ya mawasiliano ya habari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema fursa ya kuwa na huduma ya broadband katika maeneo ya vijijini duniani kote itasaidia mchakato wa haraka wa kufikia malengo ya milenia (MDG\'S).

Ban ameyasema hayo katika ujumbe wake maalumu wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya habari na mawasiliano. Ameongeza kuwa huduma ya tovuti inasaidia katika biashara, uchumi na elimu.

Ametaja pia kuwa huduma ya matibabu kwa kutumia mtandao imesaidia kuimarisha hudumu za afya, huku mitambo ya satellite ikishughulikia matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuchagiza usafi wa miji.

Kwa upande wa Umoja wa Mataifa Ban amesema umejidhatiti kuhakikisha kwamba watu wote duniani wanakuwa na fursa ya habari na teknolojia ya mawasiliano. Ameukumbusha ulimwengu umuhimu wa mawasiliano akitoa mfano wa tetemeko la ardhi Haiti, kuwa mawasilino yamesaidia sana kuratibu misaada na kuwasaidia waathirika.