Skip to main content

Wimbo wa kuchagiza malengo ya milenia umezinduliwa Afrika Kusini

Wimbo wa kuchagiza malengo ya milenia umezinduliwa Afrika Kusini

Timu ya Umoja wa Mtaifa iliyoko nchini Afrika ya Kusini imetunga wimbo maalumu wa kuchagiza malengo ya milenia kwa kushirikiana na wanamuziki maarufu barani Afrika.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Bi Helen Clark amekabidhi wimbo huo kwenye mkutano wa kuwahamasisha watu kuhusu malengo ya milenia (MDG'S) mjini Johanesberg, kampeni itakayokwenda sambamba na michuano ya kandanda ya kombe la dunia mwaka huu .

Lengo la wimbo huo ni kuchezwa na kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi wakati wa mashindano ya kombe la dunia na hivyo mashambili wataweza kuyatambua malengo ya milenia.

Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua mchakato wa kusaidia kuzuia usafirishaji haramu wa watu wakati na baada ya kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini