Mkuu wa haki za binadamu amesema ana matumaini baada ya kuzuru Japan

Mkuu wa haki za binadamu amesema ana matumaini baada ya kuzuru Japan

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amesema amekyuwa na mazungumzo yanayotia matumaini na viongozi wa Japan katika masuala mbalimbali.

Bi Pillay ambaye amehitimisha ziara yake nchini Japan amesema miongoni mwa mambo waliyojadili ni pamoja na haki za kimataifa za binadamu, kama ubaguzi, jinsi wanavyowashughulikia wahamiaji, njia za kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu, hukumu ya kifo na jinsi ya kutumia uwezo wa Japan kama mshawishi mkubwa kimataifa.

Akiwa nchini humo kwa ziara ya siku tatu Bi Pillay amezungumza na waziri mkuu bwana Yukio Hatoyama, waziri wa mambo ya nje Bwana Katsuya Okada na waziri wa sheria Bi Keiko Chiba pamoja na Bi Sadako Ogata rais wa JICA ana aliwahi kuwa kamisha wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.