Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LRA wazidi imeshambulia Sudan, DR Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati

LRA wazidi imeshambulia Sudan, DR Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepokea ripoti ya kusikitisha kwamba kumekuwepo na ongezeko la mashambulizi kutoka kwa kundi la waasi wa Uganda la Lords Resistance Army LRA.

Kundi hilo linadaiwa kuongeza mashambulizi dhidi ya raia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kundi lilo limefanya mashambulizi tarehe 20 Machi na tarehe sita ya mwezi huu wa Mai kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya kKati katika mkoa wa Haut-Mbomou vijiji vya Agoumar, Guerekindo,Kitessa na Misikine.

Katika mashambulizi hayo watu 36 wameuawa, nyumba kuchomwa moto na watu wengine 10,000 wakiachwa bila makazi. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR