Skip to main content

Chad imetoa ruksa kwa IAEA kukagua shughuli zake za nyuklia

Chad imetoa ruksa kwa IAEA kukagua shughuli zake za nyuklia

Chad imekuwa nchi ya 100 duniani kukubali kutoa taarifa zake za nyuklia kwa shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za atomic IAEA.

Shirika hilo limeipongeza hatua ya Chad na kusema ni muhimu katika jitihada za kimataifa za kukabiliana na matumizi ya nyuklia. Hatua hiyo itawaruhusu wakaguzi wa IAEA kupata taarifa zaidi na kuzuru maeneo ya shughuli za nyuklia za nchi hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano amesema ankaribisha hatua hiyo na kuyataka mataifa yote ambayo hayajafanya hivyo kuchukua hatua bila kuchelewa. Ameongeza kuwa hatua kama hiyo ni muhimu sana kwani inaisaidia IAEA kujua shughuli zote za nyuklia na kubaini kama ni za amani na kama nchi zina mitambo ya nyuklia ambayo haijulikani kimataifa.