Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM akutana na viongozi Ivory Coast kujaribu kutatua mzozo wa Kisiasa

Mjumbe wa UM akutana na viongozi Ivory Coast kujaribu kutatua mzozo wa Kisiasa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Y,J,Choi, amekutana na kiongozi wa chama cha Rally of Republicans (RDR), Alassane Dramane Quattara, ilikujadili hali katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, hususani maswala ya uchaguzi na muungano.

Baada ya mkutano wa hapo jana, Bw Choi ambaye ni mjumbe maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa muda mrefu umepita kuhusiana na maswala haya mawili na hali hii inachangia mgogoro nchini humo.

Bw Choi, ameongeza kuwa hali ilivyo kwa sasa na hasa utatuzi wa mgogoro ni nyeti. Amesema hali ya uchaguzi ni lazima itatuliwe kwa haraka kando na hatua itakayowezesha muungano, ili kwa pamoja waweze kupiga hatua katika jitahada za kumaliza mgogoro.