Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mdororo wa uchumi unatishia upungufu wa chakula Ulaya na Asia

Mdororo wa uchumi unatishia upungufu wa chakula Ulaya na Asia

Hali ya kushuka kwa uchumi duniani inatishia kurudisha nyuma mafanikio ya uchumi yaliyopatikana kw anjia ya kilimo, ili kukabiliana na umaskini na upungufu wa chakula barani Ulaya na Asia ya Kati.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) takribani watu milioni 50 wameondokana na umasikini kwanzia mwaka wa 1998. Asia ya Kati pekee idadi ya walio maskini imepungua kwa asilimia 40 hadi kufikia watu milioni sita katika kipindi cha mwaka 2004 hadi 2006.

Utafiti wa FAO umeonyesha kuwa kushuka kwa uchumi kumeathiri hali ya kilimo Ulaya na Asia ya Kati, sawa na utafiti wa Benki ya Dunia ambao unakadiria kwa eneo la limeathirika pakubwa na misukosuko ya kiuchumi duniani.