Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya kibinadamu imewafikia waathirika wa mafuriko Afghanistan

Misaada ya kibinadamu imewafikia waathirika wa mafuriko Afghanistan

Juhudi za pamoja za Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) na Mamlaka ya taifa ya Kukabiliana na majanga ya Afghanistan (ANDMA) wemewapelekea msaada kwa watu walioathirika na mafuriko Magharibi mwa Afghanistan.

Watu 70 wameuwawa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kwa mujibu wa mamlaka ya majanga ya taifa ya Afghanistan mamia ya nyumba zimeharibiwa huku maelfu ya mifugo wameuwawa. Baadhi ya misaada waliyopeleka ni pamoja na vifaa vya watoto, mablanketi, biskuti, madamu ya maji na mahema.