Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama limeongeza muda wa MINURCAT Chad na CAR

Baraza la usalama limeongeza muda wa MINURCAT Chad na CAR

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongezeka muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati MINURCAT kwa wiki mbili zaidi.

Muda huo umeongezwa huko baraza hilo likitathimini iwapo watapunguza vikosi walinda amani katika mataifa hayo.

Kikosi cha MINURCAT kilianzishwa mwaka 2007 ili kuhakikisha usalama wa maelfu ya wakimbizi wa Durfur na walioachwa bila makazi na wafanyakazi wa mashirika ya misaada katika mataifa hayo. Mahmoud Youssouf ni mwakilishi wa MINURCAT anafafanua kuhusu kuongezwa kwa muda huo.