Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa baraza la haki za binadamu umefanyika leo UM

Uchaguzi wa baraza la haki za binadamu umefanyika leo UM

Mkutano mkuu wa Umohja wa Mataifa leo unatarajiwa bila kupingwa wajumbe kutoka nchi 14 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwenye baraza la haki za binadamu.

Hata hivyo uchaguzi huo umeshaanza kuzua utata hata kabla haujafanyika kwa makundi yasio ya serekali yakidai kuwa wajumbe watano kati ya watakaochaguliwa ikiwemo Libya wana rekodi mbaya ya haki za binadamu na hawapaswi kuchaguliwa.

Katika taarifa ya pamoja ya makundi hayo likiwemo shirika la kimataifa la kupigana haki za binadamu Human Rights Watch yanasema wagombea watano wa mwaka huu Angola, Libya, Malaysia, Uganda na Thailand hawafai kuwa wajumbe wa baraza hilo. Baraza la haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini Geneva tangu lilipoanzishwa mwaka 2006 limekuwa likijaribu kuepuka utata wa aina yoyote katika utendaji wake.