Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tume ya maendeleo endelevu leo unajadili usafiri

Mkutano wa tume ya maendeleo endelevu leo unajadili usafiri

Mkutano wa ngazi ya juu wa tume ya maendeleo endelevu CSD leo umeingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Pamoja na mada mbalimbali zinazojadiliwa kwenye mkutano huo zikiwemo za mazingira na madini leo wanatoa kipaumbele kwenye suala la usafiri.

Mkutano huo unatathimini mambo mbalimbali na fursa ya kuweza kukabiliana nayo. Katika mada ya leo ambayo ni usafiri washiriki wanajadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo katika karne hii ya 21 na pia mchango wake kwa maendeleo na kufikia malengo ya milenia.