Msaada zaidi watangazwa kwa wananchi wa Haiti walioathirika na tetemeko

Msaada zaidi watangazwa kwa wananchi wa Haiti walioathirika na tetemeko

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula la Umoja wa Mataifa ( WFP) Josette Sheeran, ametangaza kuongezwa kwa mradi wa pesa na kazi, na chakula kwa wanafuzi shuleni ili kujenga raia thabiti na bora nchini Haiti.

Sheeran amesema hatua moja baada ya nyingine, watu wa Haiti wanajeng ataifa lao hii ni pongezi kwa taifa ambalo limeonyesha uvumilivu ya hali ya juu licha ya maafa mbaya mno.

Miezi minne baaday ya tetemeko la ardhi nchini Haiti, Shirika ka WFP, likishirikiana na seriklai ya nchi hiyo, wanatumia mbini mengi ikiwemo watu kupatiwa pesa baada ya kufanya kazi, watu kupewa chakula baada ya kazi, kuwapa watoto chakula shuleni, sawa na kununuliwa kwa baadhi ya mahitaji hayo ilikusadia wakuzaji wa nchini humo. Mpango huu utawanufaisha wato zaidi ya milioni mbili katika mchakato wenye nia ya kuwasaidia watu wa Haiti badala ya wao kuwategemea watu kutoka nje ya nchi