Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM kuzuru Brazili kutathimini mfumo wa utumwa wa kisasa

Afisa wa UM kuzuru Brazili kutathimini mfumo wa utumwa wa kisasa

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa, Gulnara Shahinian, atazuru nchini Brazil kuanzia tarehe 17 hadi 28 mwezi huu kwa utafiti wa kujione mwenyewe, hali halisi.

Hii ikiwa ni ziara ya kwanza kwa wataalamu huru wa baraza la haki za binadamu nchini humo, kutathimini mfumo wa utumwa wa kisasa, chanzo chake pamoja na athari zake. Bi Shahinian amesema nchi ya Brazil imetunga sheria sawa na progaramu ya kupambana na utumwa wa kisasa kama vile ajira ya lazima.

Na kuongezea kuwa ziara hii itatoa fursa muafaka ya kuthathmini na kuripoti matokeo ya juhudi hizi. Baadhi ya mifano ya dhulma za kisasa ni kama vile ajira ya lazima, utumishi wa nyumbani na ajiya mbaya ya watoto.