Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali za afikiana kutokomeza mifumo mibaya ya ajiya ya watoto duniani

Serikali za afikiana kutokomeza mifumo mibaya ya ajiya ya watoto duniani

Zaidi ya wajumbe 450 kutoka nchi 80 wanaokutana mjini Geneva kuhusu ajira kwa watoto wameafikiana kuchukua hatua kutokomeza mifumo mibaya ya ajira ya watoto ifikapo mwaka 2016.

Azimio hilo limeafikiwa wakati wakihitimisha mkutano wa siku mbili kuhusu ajira kwa watoto uliofadhiliwa na shirika la kazi duniani ILO kwa ushirikiano na serikali ya Uholanzi.

Maafikiano yao yanatoa wito kwa serikali zote, wadau mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali na jumuiya za kijamii kusisitiza uwezo wa kupata elimu, kuwalinda watoto na kuhakikisha ajira zinazotolewa ni zile zinazokubalika.