Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Afghanstan aelezea hofu juu ya ugonjwa uliowakumba wasichana wa shule

Mwakilishi wa UM Afghanstan aelezea hofu juu ya ugonjwa uliowakumba wasichana wa shule

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Stafan De Mistura ameelezea hofu yake juu ya ugonjwa wa ajabu uliowakumba wasichana wa shule nchini Afghanistan.

Taarifa kutoka mjini Kunduz, Daikundi na Kabul zinasema wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali za miji hiyo wameugua kutokana na kinachodaiwa wamedhurika na aina fulani ya kemikali.

Shirika la afya duniani WHO, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wizara za afya na elimu za Afghanistan na uongozi wa maeneo hayo wanafanya uchunguzi wa taarifa hizo, kuwasaidia kwa matibabu walioathirika na kutafuta njia za kuzuia uwezekano wa ukiuaji wa masuala ya kiusalama kwenye shule za nchi hiyo usitokee tena. Damu za wasichana hao zimechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara nje ya nchi ili kuchunguzwa na kujua nini hasa kilichowazuru.