Burundi yaonyesha ukomavu wa kisiasa ikijiandaa na uchaguzi:UM

Burundi yaonyesha ukomavu wa kisiasa ikijiandaa na uchaguzi:UM

Baada ya miongo kadhaa ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, uchaguzi ujao utaipa Burundi nafasi ya kuweka kiwango bora kipya cha amani na demokrasia katika eneo la maziwa makuu Afrika kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa nchi hiyo.

Charles Petrie ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi ametoa matamshi hayo katika taarifa yake kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Burundi. Wakati huo huo, Petrie amesema huu ni wakati wa kihistoria kwa Burundi na eneo zima, baada kumalizika kipindi cha mpito 2005, Burundi ilifanya uchaguzi ambao usababisha kuchaguliwa kwa serikali ya kidemokrasia .

Ameongezea kuwa mwaka huu , Burundi imeonyesha ukomavu wa kisiasa kwani kama taifa ambalo hadi majuzi limekabiliwa na mgogoro wa ndani, sasa lina matumaini ya kuonyesha jinsi serikali iliyochaguliwa inaweza kukabidhi mamlaka kwa mshindi wa uchaguzi .

(SAUTI Petrie:Licha ya mambo mazuri ambayo yametoke hadi sasa, na amini bado kuna changamoto chungu nzima . Hebu nilikumbushe baraza hili kwamba uchaguzi huu unaendelea huku kukiwa kumbukumbu za ghasia na mahangaiko mengi kwa raia kwa miaka ya hivi karibuni . Kwa mtazamo wangu changa moto za siku za usoni ni kuwepo na mkazo wa kalenda ya uchaguzi na utatuzi wa mgogoro utakaotokea wakati wa uchaguzi baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, na utatuzi wa mgogoro utakaotokana na uchaguzi baadae.)