Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na serikali ya Iraq wameanzima mipango kuikomboa kiuchumi Iraq

UM na serikali ya Iraq wameanzima mipango kuikomboa kiuchumi Iraq

kwa pamoja Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq wameanzisha mipango ya kuboresha utawala, huduma kwa jamii na ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano.

Hatua hiyo imekuja baada ya kutiwa saini kwa mkata ambao umetajwa kama hatua ya kihistoria kwa watu wa Iraq na Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Christine Mcnab.

Timu ya Umoja wa Mataifa iliyoko Iraq pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wadau wengine, walishiriki katika kuandaa mpango huo wa msaada wa Umoja wa Mataifa UNDAF, kwa kipindi cha 2011-2014.

Mcnab amesema kutiwa saini kwa mpango huo kutaboresha ushirikiano ambao utawaletea maendelo bora ya siku za usoni raia wa Iraq.