Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF imekabidhi mradi wa maji Kaskazini mwa Somalia kuwasaidia maelfu

UNICEF imekabidhi mradi wa maji Kaskazini mwa Somalia kuwasaidia maelfu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika juhudi za kuboresha huduma muhimu nchini Somalia limekabidhi mradi wa maji kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ili kuwapa maelfu ya watoto na familia zao maji safi ya kunywa.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF katika kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika As Sy maji ni rasimali muhimu katika maisha lakini pia yaweza kuwa chanzo cha magonjwa. Amesema hivyo ni muhimu kwa familia za maeneo hayo ya Somalia kupata maji safi na salama.

Sy ameyasema hayo baada ya kuzuru maeneo ya Bossaso katika jimbo lililojitenga la Puntland kaskazini mashariki mwa Somalia ambako mradi huo wa maji uluojengwa kwa msaada wa UNICEF umekabidhiwa rasmi.