Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAMID asisitiza usitishwaji mapigano Darfur na kuwalinda raia

Mkuu wa UNAMID asisitiza usitishwaji mapigano Darfur na kuwalinda raia

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Alain Le Roy na mjumbe wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Ibrahim Gambai wamehudhuria mkutano wa pamoja na serikali ya Sudan uliomalizika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Mkutano huo umetathimini hali ya usalama kwenye jimbo la Darfur na kulepelekwa kwa kikosi cha ziada cha UNAMID ambapo kufikia sasa asilimia 88 ya wanajeshi na asilimia 74 ya polisi wako nchini Sudan kulinda amani.

Bwana Gambari amesisitiza kwamba mambo muhimu ni kahakikisha usalama wa raia na wakimbizi wa ndani wa eneo la Darfur pamoja na kuongeza msukomo wa juhudi za kuleta amani ya kudumu. Pia kuwepo na maendeleo ya haraka katika eneo hilo na kurejesha hali ya maelewano kati ya Sudan na Chad.