Wataalamu wa UM wameonya juu ya sheria ya Arizona inayowabagua wachache

Wataalamu wa UM wameonya juu ya sheria ya Arizona inayowabagua wachache

Kundi la wataalamu wa kupigania haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo limeelezea hofu yake juu ya sheria mpya ya jimbo la Arizona hapa Marekani ambayo itawaathiri na kubagua makundi ya walio wachache, na wahamiaji.

Wataalamu hao wameonya kwamba sheria hiyo mpya ambayo tayari imeshazusha utata na kusababisha maandamano ya kuipinga, itaruhusu ubaguzi wa wachache na itawapa haki polisi ya kuchukua hatua zinazowalenga watu wachache kwa misingi ya asili yao.

Pia itaathiri mitaala ya shule kwa kuangalia historian a utamaduni wa walio wachache, hasa kama ni wahamiaji, ubaguzi wa rangi, wanatoka katika kundi gani, asili yao, elimu na haki za kitamaduni.