Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeziomba serikali za mgharibi kuwalinda wakimbizi wa Kisomali

UNHCR imeziomba serikali za mgharibi kuwalinda wakimbizi wa Kisomali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limetoa taarifa kwamba wakimbizi kutoka katikati na Kusini mwa Somalia wanahitaji ulinzi wa kimataifa.

Katika taarifa yake UNHCR imetoa mwongozo mpya wa kuwalinda maelfu ya Wasomali wanaokimbia machafuko nchini mwao. Mwongozo huo una lengo la kuzichagiza hususani serikali tajiri kutowarejesha makwao maelfu ya wakimbizi wa Kisomali wanaotafuta hifadhi bali wayafikirie maombi yao ya ukimbizi.

Yusuf Hassan ni msemaji wa UNHCR mjini Nairobi Kenya anafafanua muongozo huo mpya unasemaje kwa nchi zinazohifadhi wakimbizi.