Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa mawasiliano na teknolojia (WSIS) umeanza Geneva

Mkutano wa kimataifa wa mawasiliano na teknolojia (WSIS) umeanza Geneva

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha teknolojia ya kisasa amesema habari, mawasiliano and tekinolojia ya kisasa kama vile tovuti iliyo na kasi inaweza kusaidia katika kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi na jamii na hivyo kuchangia katika kufikiwa kwa malengo ya Milienia (MDG's) .

Akizungumaza katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mawasiliano , katibu Mkuu wa chama cha kimataifa cha wafanyi kazi wa teknolojia ya kisasa Hamadoun Toure, amesema mtandao wa Broadband unaweza bila shaka kusaidia katika kuyarejesha kwenye mstari Malengo ya Milenia.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekiri kuwa juhudi katika kuafikiwa kwa Malengo ya Milenia ifikapo 2015 zimekuwa zikienda pole pole.