Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ya Kusini kutumia kombe la dunia kendeleza vita dhidi ya ukimwi

Afrika ya Kusini kutumia kombe la dunia kendeleza vita dhidi ya ukimwi

Wakati Afrika Kusini ikijianda na Kombe la Dunia la kandanda mwaka huu, serikali ya nchi hiyo inatumia fursa hii ili kuimarisha kampeni yake ya vita dhidi ya ukimwi na ushauri kwa watu walioambukizwa virusi vya ukimwi.

Katika muda wa mwaka moja ujao, serikali imepanga zaidi ya watu millioni 15 nchini humo watapimwa na watajua hali yao ya ukimwi. Kwa mujibu wa tarakimu kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na ukimwi UNAIDS , idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi nchini Afrika ya Kusini ni milioni 5.7 ambayo ni asilimia 17 ya watu walio na Ukimwi ulimwenguni.

Nchi hiyo ina zaidi ya akina mama milioni 3.2 walioambikizwa virusi vya ukimwi huku kukiwa na watoto yatima zaidi ya millioni 1.4 . Dr Yogan Pillay ni kutoka kwa wizara ya afya nchini Afrika kusini

(SAUTI Dr Yogan :Kampeni ya ushauri na kupimwa HIV imeandaliwa kuonyesha watu kuwa hakuna haja ya kuwabeza watu walioambikizwa UKimwi. Na tunatumai viongozi wetu katika kila sekta ya jamii watachukua nafasi na kupimwa ilikujua hali yao na kama wanafursa watawaelezea wananchi hali yao , na hatua hii itasaidia katika kupunguza kunyanyapaliwa kwa watu walioambukizwa virusi vya HIV katika jamii. Na faida nyingine ya kampeni hii ya ushauri na kupimwa ni kuwa muangalifu iwapo utapatikana umeabukizwa au la, na pia kutafuta matibabu. Tumekuwa tukifanya kazi na FIFA ili kutafuta kubuni njia ya kuongeza elimu katika jamii kuhusiana na HIV na Ukimwi katika muda wote wa mashindano ya Kombe la Dunia. Na katika sekta ya Utalii tunafanya kazi na wamiliki wa mahoteli ili kuhakikisha kwamba mfano mipira ya kondomo itakuwepo kila wakati.)