Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa UNICEF ataka vijana kuchagiza amani nchini Guinea

Balozi mwema wa UNICEF ataka vijana kuchagiza amani nchini Guinea

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Mia Farrow amezindua mradi wa dola milioni 1.65 unaowalenga vijana ili kuwachagiza kuwa washiriki wa amani kwenye uchaguzi ujao nchini Guinea.

Katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana mjini Conakry Farrow amesema kufanya kazi na vinaja ili kuleta maelewno miongoni mwa jamii hasa wakati huu kabla ya uchaguzi mkuu na siku za usoni ni muhimu sana.

Mradi huo unadafadhiliwa na mfuko maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza amani kwa ushirikiano na UNICEF, shirika lisilo la kiserikali la Search for Common Ground , UNIDO na serikali ya Guinea. Mradi huo utawahusisha vijana 23,000 wa kike na wa kiume katika maeneo yaliyosahaulika katika miji ya Conakry na Forest nchini Guinea.