Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya UM inaonya juu ya athari za bayoanuai kwa maisha ya binadamu

Ripoti mpya ya UM inaonya juu ya athari za bayoanuai kwa maisha ya binadamu

Tathimini ya karibuni ya hali ya sasa ya bayoanuai na athari zake kwa maisha ya kila siku ya binadamu imedokeza kuwa mfumo asilia unaosaidia masuala ya uchumi, maisha na kuishi katika sayari hii uko katika hatari ya kuporomoka kabisa.

Tathimini hiyo inasema hadi pale kutakapokuwa na mabadiliko na hatua za ubunifu na kutumia vyema viumbe vingine basi maisha ya binadamu yataarthirika.

Katika toleo la tatu la mtazamo wa kimataifa wa byoanuai (GBO-3) lililotolewa na mkataba wa kibaolojia wa bayoanuai (CBD) limethibitisha kwamba dunia imeshindwa kwa kiasi kikubwa kutimiza lengo lake la kupunguza kiwango cha uharibifu wa bayoanuai ifikapo mwisho wa mwaka huu.